Mafanikio ya kupambana na vifo vitokanavyo na saratani ya mlango wa kizazi yanaelekea kuafanikiwa mara baada ya uzinduzi wa Chanjo ya Kinga ya saratani ya mlango wa kizazi ulifanyika katika kituo cha afya cha Town Clinic kilichopo mjini Mpanda.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi, mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ndugu Obed Mahenge alitoa ufafanuzi wa saratani ya mlango wa kizazi na kueleza kuwa Chanjo hii inayotolewa kwa watoto wa kike wenye umri kati ya miaka 14. Aidha Dkt alisema “Nchini Tanzania, saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza kwa vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti. Saratani hii husababishwa na virusi vya Papilloma (Human Papiloma Virus-HPV) ”. Pia alivitaja visababishi vya maambukizi ya virusi vya papilloma kuwa ni Kuanza kujamiana katika umri mdogo, Kuwa na wapenzi wengi, Kuwa na ndoa za mitala, Kuzaa watoto wengi na Uvutaji wa sigara.
Sambamba na visababishi hivyo alizitaja dalili za saratani hiyo kuwa niKutokwa damu bila mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiana, Maumivu ya mgongo, miguu na au kiuno, Kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa hamu ya kula, Kutokwa uchafu kwenye uke wa majimaji, uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu pamoja na Kuvimba mguu mmoja
Awali kabla ya kuzindua chanjo hiyo Mheshimiwa Mstahiki Meya alimtaka mganga mkuu kuendelea kutoa taarifa na matangazo ili wasichana wenye vigezo vya kupata chanjo hiyo ambao hawako mashuleni wapate fursa ya kupata chanjo hiyo.
Aidha aliwaomba wazazi wawe na tabia ya kupima mara kwa mara ili kuijua afya yao na kuchukua hatua haraka mara wanapogundulika kuwa na visahiria au dalili za saratani ya shingo ya kizazi.
Pia aliwaomba wazazi waondoe shaka dhidi ya chacho hiyo kuwa ni salama na haina madhara yoyote kwa mtumiaji, hivyo aliwaomba wazazi wawaruhusu watoto wao ili wakapate chanjo hiyo.
Katika uzinduzi uliofanyika siku hii ambayo pia ilikuwa ni siku ya Malaria duniani, Mheshimiwa mstahiki Meya aligawa vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto walikuwa wamekuja kliniki ikiwa ni ishara ya Manispaa kupinga na kuwalinda wananchi juu ya ugonjwa wa maralia.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.