WASAFIRI WAHESABIWA
Baadhi ya wananchi waliokuwa wakisafiri kuelekea maeneo mbalimbali nchini kutokea mkoani Katavi usiku wa kuamkia tarehe 23/08/2022 wamehesabiwa wakiwa katika stendi ya mabasi ya Mizengo Pinda iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Wasafiri hao wameipongeza serikali kwa namna ilivyoratibu zoezi la Sensa kwa mwaka huu ambapo makarani walifika stendi ya mabasi ya Mizengo Pinda mapema na kutoa utaratibu mzuri wa kuanza kuwahesabu abilia wote walikuwa wanatarajia kusafiri alafajiri ya tarehe 23/08/2022.
Wakizungumza baada ya kuhesabiwa katika stendi kuu ya mabasi ya Mizengo Pinda wamesema Sensa ya mwaka huu imekuwa na hamasa kubwa na hata zoezi lenyewe linaendeshwa kisasa.
-
"Mimi binafsi nimehesabiwa hapa stendi na nimefurahi zoezi lilivyoenda, niwashauri tu wale ambao bado hawajafikiwa wasiwe na hofu kwani zoezi hili linaendeshwa kisasa na kingine niwaombe kutoficha taarifa," amesema Specioza Daniel.
Kwa upande wake mratibu wa Sensa Manispaa ya Mpanda, Paul Kahoya ambaye aliambatana na makarani usiku amesema zoezi limeenda kama lilivyopangwa na kuongeza kuwa ni imani yake kuwa litakamilika kwa utaratibu uliowekwa.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.