WASINDIKAJI WAWESHWA MIUNDOMBINU NA MASHINE
Bi Cresensia Joseph kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko amefungua rasmi jengo la wasindikaji wa bidhaa mbalimbali lilopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda lililojengwa chini ya mradi wa Kilimo Bora cha Mboga na Matunda kwa Wanawake na Vijana KIBOWAVI chini ya AGRI - CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU). Ufunguzi wa jingo hilo umefanyika 16 Novemba 2022.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi na ununuzi wa mashine za viliyogarimu zaidi ya milioni 200 afisa maendeleo ya jamii Bi Maritha Mlozi alieleza kuwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kushirikiana na Umoja wa Wasindikaji wa Mboga na Matunda (UWAMBOMAKA) iliwasilisha ombi la uwezeshwaji katika maeneo ya kuboresha majengo, mafunzo na vifaa kwa ajili ya shughuli za uzalishaji na usindikaji, kwenda mradi wa Kilimo Bora cha Mboga na Matunda kwa Wanawake na Vijana (KIBOWAVI) chini ya AGRI – CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU). Hii ilitokana na changamoto walizokuwa wanapitia wasindikaji kutokana na kusindika kienyeji bidhaa mbalimbali za chakula majumbani ambako mazingira yalikuwa siyo rafiki kiafya na kutoruhusu wasindikaji kupata nembo za ubora (TBS).
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda bi Sophia Kumbuli amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutafuta wafadhili ambao wamewezesha ujenzi na ukarabati nua ununuzi wa mashine mbalimbali ambazo zitarahisisha na kuongeza thamani na uzalishaji katika shughuli za wajasiliamali.
Akiwasilisha hotuba ya mkuu wa mkoa wa katavi Bi Cresensia Joseph kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa katavi amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuilinda miundombinu, mashine na kuendeleza yote ambayo ya yamejengwa katika kiwanda ambacho kimezinduliwa.
“Kujengewa miundombinu, kununua mashine na kupewa mafunzo ni jambo moja, jambo lililopo mbele yetu ni kuhakikisha yote yaliyoanzishwa na kufadhiliwa na wafadhili yanaendelea, kwa kweli sitegemei kukuta kiwanda hiki kilichosheheni mitambo kimetelekezwa na hakifanyi kazi.” Alisema Bi Cresensia Joseph kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Katavi
Aidha Bi Sophia amemshukuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta wafaddhili, pia amelishukuru shirika la HELVETAS - TANZANIA kupitia mradi wa KIBOWAVI chini ya AGRI - CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuwawezesha wajasiriamali kuwapatia mafunzo, vifaa, mashine na kuwaboresha mazingira ya usindikaji, uwezeshaji huu utaongeza thamani wa bidhaa, utaboresha masoko na hivyo kuwaongezea kipato.
“Tunamshuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea wafadhili, pia Tunalishukuru sana shirika la HELVETAS - TANZANIA kupitia mradi wa KIBOWAVI chini ya AGRI - CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) ambao wametufadhili ujenzi wa majengo mapya na ukarabati wa majengo ya zamani kama yafuatayo; Duka la kuuzia (Supermarket),Jengo la kutengenezea juice na matunda, Jiko, Vyumba 2 vya kubadilishia nguo, Vyoo 2, Mtambo wa kusindika Wine, Mashine za kusagia unga wa lishe na viungo, Chumba cha kusagia, Mashine ya kukata viungo, Freezer 2, Mfumo wa umeme wa jua, Uzio, Kaushio (solar drier), Shelves, CCTV CAMERA 15 ambavyo vyote kwa pamoja vimegharimu zaidi ya shilingi milioni 200” . Alisema Maritha Mlozi kwa niaba ya Mkurugenzi
Bi Sophia amemuhakikishia mwakiliahi wa Mkuu Mkoa wa Katavi kuwa Manispaa ya Mpanda itailinda miundombinu yote iliyojengwa na mashine zote zilizonunuliwa kwa ajili ya kuwawezesha wasindikaji. Aidha Manispaa itaendelea kushirikiana na Umoja wa Wasindikaji wa Mboga na Matunda (UWAMBOMAKA) pamoja na wadau wote ili kuhakiksha tija ya kiwanda iliyokusudiwa inapatiaka.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.